NA C4C
Hivi sasa ambapo watoto wengi wapo nyumbani badala ya mashuleni ili kuzuia kuenea kwa maambukizi ya Covid19, majukumu ya shule na waalimu sasa yamewaangukia wazazi. Kama shirika ambalo linaelewa umuhimu wa elimu katika makuzi ya watoto, tunapenda kutoa mwongozo wa baadhi ya njia muhimu ambazo unaweza kutumia wewe na mtoto wako katika kujifunza wakati huu.
Pamoja na kutumia njia hizi tunashauri pia yafuatayo:
Zingatia ratiba ya kila siku kwani inawasaidia watoto, haswa katika kipindi hichi cha wasiwasi.
Usiwanyime fursa ya kucheza na kufurahi (hii inapaswa kuendelea kufanyika kama ilivyo sehemu ya siku yao wawapo shuleni)
Tumia vizuri rasilimali na muda ulionao. Mzazi usiteseke kutamani kutimiza malengo yasiyowezekana ya watoto kujisomea nyumbani, Kujipa mawazo yasiyo ya lazima kunaweza kuathiri familia nzima kipindi hichi ambapo tayari kuna mtafaruku.
Shule Direct: Hutoa nyenzo za kujifunzia mtandaoni kwa wanafunzi wa shule za sekondari, kutoka kidato cha kwanza hadi kidato cha nne. Baadhi ya nyenzo hizo ni notes za masomo yaliyo ndani na nje ya mtaala wa elimu. Pia hutumia teknolojia kutoa majibu ya papo hapo kwa maswali mbalimbali yaliyoulizwa na wanafunzi. Katika kipindi hiki ambapo shule zimefungwa, wameandaa mitihani ya nusu muhula kwa wanafunzi wa sekondari kujipima. Unaweza kutumia Shule Direct kupitia application yao kwenye simu yako ya mkononi, pia kupitia tovuti yao ya https://www.shuledirect.co.tz/ kwa Tanzania na https://www.shuledirect.co.ke/ kwa Kenya.
Ubongo Toolkits:Wanaandaa nyenzo za kujifunzia katika mfumo wa katuni na makala mbalimbali zilizo rafiki kwa watoto wenye umri wa miaka 0-14 ambazo zinawafundisha watoto kuhesabu, kuandika, ustadi katika ufundi, sayansi na teknolojia. Hivi karibuni wameongeza mafunzo juu ya afya na usafi kwa watoto kama njia ya kuzuia maambukizi ya COVID-19 na pia mafunzo juu ya ushiriki wa walezi katika malezi na utoaji wa elimu kwa watoto. Unaweza kupata mafunzo hayo kupitia tovuti yao, http://toolkits.ubungo.org/ pia kwa kujiunga na kundi la Whatsapp kwa ajili ya kupata nyenzo mbalimbali. Unaweza pia kufuatilia vipindi vyao vinayorushwa hewani kupitia TBC1 kila Jumatatu hadi Ijumaa saa nane na nusu mchana, na Jumamosi na Jumapili saa tatu kamili asubuhi. Unaweza pia kufuatilia vipindi vyao vinavyo rushwa hewani kupitia EATV, Azam TV na stesheni za radio 11 nchini. Kufahamu zaidi juuu ya ratiba zao za vipindi, tembelea hapa: https://www.ubongo.org/
MTABE: Hutumia teknolojia kutoa majibu ya papo hapo yanayolingana na mtaala wa elimu kwa wanafunzi wa shule za sekondari kuazia kidato cha kwanza hadi cha kidato cha nne. Pia wanatoa matirio na mitihani ya masomo mbalimbali. Kwa sasa, unaweza kupata huduma zao kupitia programu ya simu za androids Ili kuwafikia wanafunzi wengi zaidi, hivi karibuni watazindua njia mpya ya kutumia huduma zao kupitia Telegram na WhatsApp na pia wataboresha na kuzindua upya huduma yao kwa njia ya ujumbe mfupi. Tembelea tovuti yao kufahamu zaidi: https://mtabeapp.com/
SmartClass: Ni jukwaa la mtandaoni linalounganisha wanafunzi na waalimu waliobobea na kuthibitishwa, wanaofundisha mtandaoni na ana kwa ana. SmartClass hufanya hivyo kwa kutumia teknolojia inayo chambua na kulinganisha uhitaji wa mwanafunzi na uwezo na uwepo wa mwalimu. Kutumia huduma hii, tembelea tovuti yao: https://www.smartclass-tz.com/
Comentarios