top of page

Kuunda jamil ya walinzi wa watoto kwa njia ya mtandao

Updated: Oct 13, 2022

Na Njeri Omesa


Jamii ya wana Citizens4Change imejikita katika kushirkiana na watu katika jamii, Tunaamini kwamba ikiwa kila mtoto atakuwa na mtu mkubwa anayeaminika kuwajali na kuwalinda, kutaongeza mtandao wa ulinzi kwa watoto, na kuwapa mfumo wa kuwakinga na hatari.


Tumejenga hii jamii kwa kushirikiana ana kwa ana kwa ana na wananchi kupitia vikao, tafiti na mijadala. Katika vipindi hivyi, wananchi walipata nafasi ya kujadiliana kuhusu mambo yanayo wasumbua zaidi katika kuwaweka katika jamii yao salama dhidi ya hatari. Mikutano hii ya ana kwa ana iliandaliwa ili kuweza kuwatambua walinzi wa watoto, kuweka mazingira salama ya kujifunza, na kuchochea hatua wanazochukua walinzi wa watoto ili kupunguza vitendo vya hatari kwa watoto katika jamii. Pia tunatumia jumbe fupi na mitandao ya kijamii kusikia mambo mbalimbali kutoka kwa wanajamii, kushirikishana maarifa na kusherehekea hatua za wanajamii katika masuala yanayohusu ulinzi kwa Watoto.


Hata hivyo, kutokana na ugonjwa wa virusi vya Corona na vizuizi kote ulimwenguni vilivyoweka kukabiliana na kuenea kwake, C4C ilibidi kubadilisha uelekeo wake ili kuwaleta watu pamoja kwenye mijadala ya mtandaoni. Kwa sasa mikutano ya kila mwezi ya wanajamii hufanyika kupitia Zoom – ambapo wanajamii hutushirikisha wasiwasi wao lakini pia kile kinachowapa matumaini linapokuja suala zima la ulinzi kwa watoto katika wakati huu mgumu. Mikutano hii ya kijamii pia imekuwa sehemu ambapo C4C wamekuwa wakileta utata wanaokabiliana nao na jamii kwa pamoja hutoa suluhisho na njia bora za kukabiliana nazo.


Tumeunda aina mbili ya mikutano kwa njia ya mtandao, ya kwanza ni mkutano wa kila mwezi wa kirafiki na wanajamii. Na aina ya pili ni mkutano wa kujifunza ambao hufanyika kila baada ya wiki sita ambapo tunaangazia kujadili masuala ya Watoto yanayojitokeza kwa undani Zaidi. Mkutano kama huu ulifanyika hivi karibuni kuadhimisha siku ya mtoto wa Afrikatarehe 16/06 ambapo tulijadili kwa kina kuhusu kauli mbiu ya mwaka huu juu ya upatikanaji wa mifumo rafiki ya haki kwa watoto.


Mikutano hii kwa njia ya mtandao inatusaidia kujifunza kuhusu wanachokipitia wanajamii wetu, kutoa fursa ya majadiliano kwa kina, ushiriki na uhamasishaji (kupitia mitandao yetu ya kijamii) katika masuala yenye manufaa kwa wanajamii wetu. Miongozo ya majukwaa haya ya kujifunza inahitaji maswali yaliyofikiriwa kwa kina ambayo yataweza kuwafanya washiriki kuelezea kile wanachokipitia na kutoa mawazo mapya na mbinu mpya za kukabiliana na changamoto zinazowakumba katika kuwaweka watoto salama.


Kama ilivyo katika kila jambo, kuna changamoto katika kujenga jamii ya mtandaoni. Changamoto kubwa imekuwa katika matumizi ya kiteknolojia kwani inalazimu washiriki kuwa na mtandao imara. Kwa usalama, inashauriwa kuwa washiriki wawashe kamera kuonyesah video zao wakati wa kikao, lakini wengi wana mtandao usio imara, na kufanya hili lisiwezekane mara zote. Hii pia Huleta changamoto pale mshiriki anapotaka kuchangia mada, lakini bado unakuta mtandao wao unasumbua. Tunakabiliana na hili kwa kutumia njia ya kutuma ujumbe mfupi, kupata mtazamo, maswali n ahata kushirkisha baadhi ya nyenzo zinazoweza kusaidia katika majadiliano, mwezeshaji hayo yote kwa sauti.


Tuna nia ya kutengeneza njia nzuri ambayo itamwezesha washiriki kuweza kutoa maoni na mitazamo yao katika kuleta mabadiliko. Tunahamasisha kila mmoja aweze kuchangia, lakini pia kutoa fursa kwa wale wanaopenda kushiriki kwa kusikiliza tu kuweza kufanya hivyo. Changamoto nyingine kubwa tuliyokumbana nayo ni suala la muda. Katika kipindi hiki ambapo kuna vizuizi vya kukutana ana kwa ana, wengi wanafurahia fursa hii ya “kupata kikombe cha kahawa mtandaoni na wana C4C wengine” na kila mara tunajikuta tunaenda zaidi ya muda uliopangwa kadri mazungumzo yanavyozidi kupamba moto. Hata hivyo hii inaonyesha watu wengi wanapendezwa na hizi fursa za mikutano kwa njia ya mtandao na wana mengi ya kueleza.

3 views0 comments

Comments


bottom of page